Wizara ya Mambo ya Ndani a Uratibu wa Serikali ya Kitaifa
Idara ya Huduma za Marekebisho
MPANGILIO WA UTOAJI WA HUDUMA KWA RAIA
Idara ya Huduma za Marekebisho inalenga kutoa huduma kwa ubora na ufanisi.
RUWAZA:
Kuwa shirika bora katika huduma za marekebisho.
LENGO:
Kukuza jamii salama na yenye haki kupitia kwa usimamizi bora wa wahalifu na utoaji wa haki.
MAADILI YA KIMSINGI:
Utaalamu, Uwazi na Uwajibikaji, Uadilifu, Usiri, Haki, Heshima kwa utu na Ushirikiano.
Maadili haya ya kinsingi yamelinganishwa na Maadili na Kanuni za Kitaifa Kuhusu Uongozi
Viwango Vyetu vya Huduma
Nambari |
Huduma Zetu |
Wajibu wako |
Malipo |
Muda |
1 |
Maswali |
Kutembelea ofisi zetu, kupiga simu au kutuma baruapepe |
Bure |
Dakika 5 |
2 |
Kujibu mawasiliano |
Kutuma mawasiliano ya maandishi |
Bure |
Siku 5 za kazi |
3 |
Kukiri kupokea mawasiliano |
Kutuma mawasiliano ya maandishi |
Bure |
Siku 3 za kazi |
4 |
Kuajiri maafisa wa magereza |
Vyeti vya kielimu na kitaaluma, kitambulisho cha kitaifa, cheti cha mwenendo mwema na cheti cha kuzaliwa |
Bure |
Siku 1 jinsi ilivyotangazwa katika hatua za kuajiri |
5 |
Kuwatembelea wafungwa: a) Wafungwa waliohukumiwa tayari b) Wafungwa wanaosubiri hukumu |
Kutembelea ofisi zetu, kuonyesha kitambulisho cha kitaifa au pasipoti wakati wa ziara |
Bure |
a) Dakika 10 kwa wafungwa waliohukumi- wa tayari b) Dakika 15 kwa wafungwa wanaosubiri hukumu |
6 |
Ripoti za uchunguzi wa kijamii kwa mahakama na taasisi nyingine za marekebisho |
a) Amri ya mahakama b) Maombi kutoka kwa taasisi nyingine za marekebisho |
Bure |
a) Siku 14 kwa amri ya mahakama b) Siku 30 kwa maombi kutoka kwa taasisi nyingine za marekebisho |
7 |
Usimamizi wa wahalifu wasio- fungwa gerezani |
Amri kutoka kwa mahakama na taasisi nyingine za marekebisho |
Bure |
Kulingana na amri ya mahakama na leseni ya kuachiliwa huru |
8 |
Utoaji wa idhini ya kutumia fedha (AIEs) |
a) Maandalizi katika idara mbalimbali |
Bure |
Siku 7 za kazi |
b) Kupata idhinisho kutoka kwa idara ya fedha |
Bure |
Siku 3 za kazi |
||
c) Ofisi ya akaunti kutoa malipo ya AIE |
Bure |
Siku 5 za kazi |
||
9 |
Kutayarisha maombi na kandarasi |
a) Kamati ya kutathmini zabuni katika idara |
Bure |
Siku 30 za kazi |
b) Taarifa inayoonyesha uwasilishaji wa LPO/LSO, ankara ya S13 na stakabadhi nyingine saidizi |
Bure |
Siku 7 za kazi |
||
10 |
Kulipia bidhaa zilizowasilishwa, huduma zilizotolewa na kazi zilizofanywa |
a) Kutayarisha mchakato wa malipo |
Bure |
Siku 5 za kazi |
b) Kutekeleza mchakato wa shughuli za benki kupitia kwa mtandao |
Bure |
Siku 2 za kazi |
||
11 |
Utoaji wa huduma za kisheria |
Kutoa ripoti rasmi ya suala au masuala ya kisheria |
Bure |
Ndani ya saa 24 |
12 |
Taarifa kuhusu matangazo ya nafasi za kazi |
Kutuma maombi na kuwasilisha vyeti vya kielimu na kitaaluma |
Bure |
Ndani ya muda wa matangazo wa siku 21 za kazi |
Ili kutusaidia kuboresha utoaji wa huduma, mawasiliano/malalamishi na maswali yanaweza kutumwa kwa anwani hii:
Katibu Mkuu, Idara ya Huduma za Marekebisho, Jumba la Telposta, Ghorofa ya 28, Mrengo wa C – Kwenye Kiingilio, Barabara ya Kenyatta, S.L.P. 30478 – 00100 Nairobi.
Anwani Zetu
Katibu Mkuu,Idara ya Huduma za Marekebisho,Jumba la Telposta, Ghorofa ya 28, Mrengo wa C – Kwenye Kiingilio, Barabara ya Kenyatta, S.L.P. 30478 – 00100, NAIROBI.Simu: +254-020-2228411Baruapepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.@correctionalKE@prisonsKE@probationKE | Waziri,Wizara ya Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Jumba la Harambee, Ghorofa ya 6, Barabara ya Harambee, S.L.P. 30510 – 00100, NAIROBI.Simu: +254-020-2227411Baruapepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.@interiorKE | Afisa Mkuu Mtendaji, Tume ya Utoaji wa Haki,Jumba la West End, Ghorofa ya 2, Mkabala wa Shule ya Upili ya Aga Khan, Barabara ya Waiyaki – Westlands,S.L.P. 20414 – 00200, NAIROBI.Simu: +254-20-270000 / 2303000 / 2603765 / 2409574 / 0777125818 / 0800221349 (Bila malipo) Baruapepe: iThis email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. |